Kikelabit

Kikelabit ni lugha ya Kiaustronesia nchini Malaysia na Indonesia inayozungumzwa na Wakelabit kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2011 idadi ya wasemaji wa Kikelabit nchini Malaysia imehesabiwa kuwa watu 4000. Pia kuna wasemaji 640 nchini Indonesia (2000). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikelabit iko katika kundi la Kiborneo-Kaskazini.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search